UKAMATAJI USIOFUATA SHERIA:
Ukamataji Usiofuata SHERIA ni MSIBA katika nchi inayofuata UTAWALA WA SHERIA. Ni muhimu sana ZAKARIA OBADI atendewe HAKI bila kujali ITIKADI yake ya Kisiasa. HAKI HUINUA TAIFA.
ELIMU YA MAADILI YA MAWAKILI:
Chonde, chonde jamani, tarehe 27 Oktoba 2026 MSIKOSE KUFIKA Mahakama ya Rufani ya Tanzania-Dar es Salaam kwa ajili ya kupata ELIMU YA MAADILI YA MAWAKILI. Si WAMEYATAKA WENYEWE?👇😂😂
TAARIFA KWA UMMA:
Tarehe 27 Oktoba 2026 nitakuwa MAHAKAMA YA RUFANI YA TANZANIA- DAR ES SALAAM, kwa ajili ya KUFUNDISHA ELIMU YA MAADILI kwa KAMATI YA MAADILI YA MAWAKILI. Nataka TUHESHIMIANE bila SHURUTI 👇
KAMATI YA MAADILI KUKAMATWA NA POLISI:
Kuna uwezekano mkubwa wa Kamati ya Maadili ya Mawakili, KUKAMATWA NA POLISI KWA KUDHARAU MAHAKAMA. Kama Kamati HAIJUI hilo, basi, IMUULIZE Peter Madeleka ambaye ANA KESI YA KUDHARAU MAHAKAMA.😂😂
INASHANGAZA SANA:
Yaani, Kesi ilipangwa KUSIKILIZWA kwa njia ya MDOMO (Oral Hearing) leo tarehe 19 Oktoba 2026. Upande wa Jamhuri WAMECHELEWA kufika MAHAKAMANI. Baada ya MAWAKILI WA SERIKALI WATATU kufika, Mheshimiwa JAJI akatoa AMRI kwamba; KESI ISIKILIZWE KWA MAANDISHI.😂😂
NIMEULIZWA HIVI:
“Madeleka, kwa nini UNAWASHINDA Mawakili wa Serikali kwenye kesi nyingi za JINAI?”.
NIMEJIBU HIVI:
“Kwa sababu, wao huwa wanaendesha kesi kwa lengo la KUKOMOA na SIYO KUTENDA HAKI kwa mujibu wa SHERIA”.
LEO KAZI NI MOJA TU:
Leo tarehe 19 Oktoba 2026, KAZI NI MOJA TU, kuhakikisha ELIMU YA “CRIMINAL REVISION” inaeleweka kwa WALE WASIOJUA. Wahi SITI YAKO MAPEMA. Chakula na Vinywaji vitatolewa BURE kama KAWAIDA 👇
TAARIFA KWA UMMA:
Kesho tarehe 19 Oktoba 2026 nitakuwa Mahakama Kuu ya Tanzania-Dar es Salaam kwa ajili ya KUFUNDISHA SHULE YA “CRIMINAL REVISION” kwa WALE WASIOJUA 👇. Hakuna KIINGILIO. Wote MNAKARIBISHWA. Chakula na Vinywaji ni BURE kama KAWAIDA.
UMOJA NI NGUVU:
Shambulio dhidi ya MMOJA WETU, ni Shambulio dhidi YETU SOTE. Wakili @Mwabuk2Boniface HAKUJICHAGUA kuwa RAIS wa TLS, bali TULIMCHAGUA. Vile vile, HAKUJITUMA kutusemea MAMBO YETU, bali, TULIMTUMA. Basi, ni wajibu wetu KUMLINDA na KUMPIGANIA.
MDAHALO KATI YA MADELEKA NA DPP:
Licha ya kuwepo TAARIFA zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, binafsi SINA taarifa RASMI kuhusu uwepo wa MDAHALO huo kati ya PETER MADELEKA na DPP. Ikiwa NITAALIKWA, nipo TAYARI KUSHIRIKI kwa maslahi ya UTAWALA WA SHERIA.