Jeshi la Polisi wilaya ya Kahama linamshikilia Katibu wa Kanda ya Victoria Zacharia Obad baada ya kuvamia nyumbani kwake jana usiku majira ya saa nane kwa tuhuma ambazo bado hazijajulikana.
Kwa sasa, Zacharia Obad yupo kituo cha Polisi Kahama, akisubiri kuchukuliwa maelezo.
Wakili Alex Dotto Massaba yupo mjini Kahama kutoa msaada wa kisheria kwa Obad.
Obad Zacharia ni kiongozi mkubwa, angeitwa Polisi kama wanashida naye angefika kuliko kutumia utaratibu wa kuvamia makazi yake Kahama mjini usiku wa manane na kusababisha taharuki.
Obad zqcharia anakuwa mwanachama wa tano, kukamatwa ndani ya kipindi kifupi. Wengine waliokamatwa na Polisi ni Mkurugenzi wa Organization na Mafunzo John Justine Pambalu, aliyekamatwa Arusha na kusafurishwa hadi Dar.
Wengine ni Mwenyekiti Bavicha Mkoa wa Kigoma Coletha Ntidyicha aliyekamatwa Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Bavicha kanda ya Victoria Fred Masele, aliyekamatwa Mwanza , Edson Malyo Mliyinga huyu alikamatwa mkoani Iringa, Fadhili Benedict Mbeya alikamatwa Dar Es salaam na Doris Msigwa aliyekamatwa Arusha.
Tafadhali, watuhumiwa hawa wafikishwe Mahakamani kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.